Loading...

AMBER ROSE NA NICKI MINAJ WAKITIFUA MTANDAONI

MWANAMITINDO, sosholaiti na muuza nyago kwenye video za muziki, Amber Rose amemtibua staa wa kike wa Muziki wa Hip Hop, Onika Tanya Maraj ‘Nicki Minaj’ baada ya kuposti picha akiwa na wigi feki.

Kupitia Mtandao wa Snapchat, Amber aliposti picha akiwa amevalia wigi feki huku akiwa amefanana na Nicki kwa kiasi kikubwa kisha akaandika ‘caption’ yenye tusi la kujichukia.

Hata hivyo, taarifa za kuposti picha hiyo zilimfiki
Loading...
bidada Nicki ambapo aliandika kwa hasira kwenye Snapchat yake.

"Amber acha kunifuatilia. Nitakuona kwenye Coachella. Huwezi kuwa na nguvu kama hizi." Kisha akaunganisha na picha.

Inaelezwa kuwa chanzo cha bifu kilianza mwaka 2010 ambapo Nicki alimuimba Amber katika wimbo wake wa Monster.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

AMBER ROSE NA NICKI MINAJ WAKITIFUA MTANDAONI AMBER ROSE NA NICKI MINAJ WAKITIFUA MTANDAONI Reviewed by By News Reporter on 5/06/2018 09:26:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.