Loading...

'BABA ALIAGA DUNIA AKIWA ANASIKILIZA MUZIKI WANGU' - ANGELLA

Loading...
Mwanamuziki Angella Katatumba ambaye kwa sasa anafanya vizuri nchini Uganda kwa vibao vyake viwili vyenye miondoko ya Kijamaica Kuzi Kz amefunguka kwamba baba yake mzazi, Bonney Katatumba alifariki akiwa anasikiliza nyimbo yake.

Akizungumza wakati wa mahojiano na radio ya Sanyu FM, usiku wa Jumamosi iliyopita, mwimbaji huyo alisema usiku wa kifo chake, Bonney alimwambia anataka kusikiliza mziki. Ndipo alipompatia muziki wake na kumuomba ausikilize.

Aliendelea kumuwekea nyimbo zake na kuzifanya zijirudie rudie. "Na ndio ulikuwa usiku wa kifo chake wakati aliposikiliza nyimbo zangu kwa kujirudia rudia. Asubuhi alipoamka tuliambiwa amepoteza maisha...RIP"

Mfanyabiashara mkubwa na maarufu nchini Uganda Bonney Katatumba, ambaye alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya Kansa baada ya kugundulika mwezi Februari na alikuwa mkarimu sana kama alivyomuelezea Angella.

Angela anajulikana kwa nyimbo zake kama Mulago Yaffe, Multiply, So Close, The Struggle na nyimbo yake mpya ya Out of my head.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
'BABA ALIAGA DUNIA AKIWA ANASIKILIZA MUZIKI WANGU' - ANGELLA 'BABA ALIAGA DUNIA AKIWA ANASIKILIZA MUZIKI WANGU' - ANGELLA Reviewed by By News Reporter on 5/08/2018 10:25:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.