Loading...

ZAIDI YA WATU 100 WAFIKISHWA HOSPITALINI KWA KULA NYAMA ISIYO SALAMA

Loading...
Watu zaidi ya 100 kutoka katika kijiji cha Kiptoror kata ya Kuresoi Kaskazini nchini Kenya wamejikuta wakikimbizwa hospitali baada ya kupata madhara kwa kula nyama iliyosemekana sio salama kwa binadamu.

Watu takriban 130 - 25 wanaume, 45 wanawake na 60 ni vijana - walifika wenyewe hospitalini wakiwa wanaharisha, wanaumwa matumbo na kupata maumivu makali ya kichwa.

Wanakijiji walisema kuwa watu hao walinunua nyama kutoka kwa mmiliki wa ng'ombe aliyekufa kwa kuwa iliuzwa bei rahisi ya Sh200 kwa kilo pesa za Kikenya.

Mkuu wa kata hiyo, Felix Wafula alisema waasirika walikula nyama hiyo ya ng'ombe Alhamisi ya wiki jana.

Daktari wa mifugo, Thomas Cheruiyot alisema ng'ombe huyo kabla ya kufa aliumwa mara kadhaa ila hakusema ni ugonjwa gani.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ZAIDI YA WATU 100 WAFIKISHWA HOSPITALINI KWA KULA NYAMA ISIYO SALAMA ZAIDI YA WATU 100 WAFIKISHWA HOSPITALINI KWA KULA NYAMA ISIYO SALAMA Reviewed by By News Reporter on 5/08/2018 09:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.