Loading...

BWAWA LAVUNJA KINGO NA KUUA WATU WENGI KENYA

Loading...
Watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha na zaidi ya 40 kujeruhiwa baada ya kuvunjika kwa kingo za bwawa la maji katika eneo la Solai katika Kata ya Nakuru, karibu Kilomita 200 Kaskazini mwa jiji kuu Nairobi nchini Kenya.

Janga hilo lilitokea usiku wa Jumatano kuamkia jana Alhamisi wiki hii, wakati wakazi wa Solai walipokuwa majumbani mwao, wengi wakiwa wamelala wakati waliposombwa na maji.

Watoto ni miongoni mwa watu walipoteza maisha katika janga hilo baya kuwahi kutokea nchini humo, na limetokea wakati huu, nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Awali Gavana wa mkoa wa Nakuru alisema kiwango cha uharibifu kinaendelea kutathminiwa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limetangaza kwenye Twitter kwamba limewaokoa watu 39.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BWAWA LAVUNJA KINGO NA KUUA WATU WENGI KENYA BWAWA LAVUNJA KINGO NA KUUA WATU WENGI KENYA Reviewed by By News Reporter on 5/11/2018 05:09:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.