Loading...

FISI 12 WALA WATU WAUAWA, MMOJA AKUTWA NA SHANGA

Loading...
Siku chache baada ya mtoto wa miaka sita, Martha Simon mkazi wa Mwaniko wilayani hapa mkoani Mwanza kuliwa na fisi, wawindaji wa jadi kutoka vijiji vya Sumbugu na Ilujamate Wilayani Misungwi, wamefanikiwa kuwaua wanyama hao 12 huku mmoja akikutwa na shanga kiunoni.

Wawili kati ya fisi hao ni watoto ambao walinaswa wakiwa hai. Martha, mwanafunzi huyo wa chekechea Shule ya Msingi Mwaniko, aliliwa na fisi Aprili 25 alipokuwa amekwenda kujisaidia baada ya kumaliza chakula cha usiku.

Baada ya msako wa fisi hao, yalipatikana mabaki ya mguu mmoja na kipande kidogo cha utumbo vilivyofanyiwa maziko.

Baada ya tukio hilo, kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji hicho chini ya mwenyekiti wao, Samwel Welesi walikubaliana kutafuta wawindaji wa jadi wenye ujuzi wa kuwaua wanyama hao na kuanza kila kaya kuchangia Sh1,500 ili kufanikisha kazi hiyo.

“Kikundi hiki kilitaka Sh1 milioni, ikabidi kila kaya ichangie Sh1,500 kutokana na ukubwa wa tatizo hilo wananchi walihamasika na hatimaye matunda yake yamepatikana,” alisema.

Kiongozi wa wawindaji hao, Ngubila Manigwa, alisema walifika kijijini hapo juzi wakiwa 80 na mbwa 90, walifanikiwa kuwaua fisi 10 huku mmoja kati yao akikutwa na shanga kiunoni na kuvinasa vitoto viwili vya wanyama hao.

“Mpaka kufikia leo (juzi) tumeua fisi 10 na watoto wao wawili, msako unaendelea tutahakikisha tunawasambatarisha wote ili kurejesha amani kwenye kijiji hiki,” alisema Manigwa.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
FISI 12 WALA WATU WAUAWA, MMOJA AKUTWA NA SHANGA FISI 12 WALA WATU WAUAWA, MMOJA AKUTWA NA SHANGA Reviewed by By News Reporter on 5/14/2018 09:54:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.