Loading...
Rais John Magufuli jana amekabidhiwa ripoti na tume iliyohakiki mali za CCM katika ofisi ndogo ya CCM, Lumumba jijini hapa.
Tume hiyo iliyoongozwa na Dk Bashiru Ally, imefanya kazi kwa miezi mitano.
“Huwezi ukaanza kupiga vita rushwa na ufisadi ndani ya Serikali wakati chama kina rushwa na ufisadi, chama nacho tunataka tukisafishe, mambo ya rushwa na ufisadi yaishe ili Tanzania iende vizuri, ndio maana tumeunda tume,’’amesema Rais Magufuli.
Rais amesema tume hiyo imefanya kazi nzuri na akaongeza kuwa ripoti hiyo itapelekwa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ndani ya mwezi huu ili ijadiliwe na viongozi watoe maelekezo.
Kadhalika, Rais Magufuli aliwaagiza wajumbe wa sekretarieti ya CCM waliohudhuria wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo kuanza kufanyia kazi baadhi ya mambo yaliyo ndani ya uwezo wao na kwamba masuala mengine yataamuliwa na vikao vikuu vya chama.
Pamoja na maagizo hayo, Rais Magufuli aliipongeza tume hiyo kwa kazi waliyoifanya na kusema kuwa alijua tume hiyo watapata shida kuwahoji baadhi ya watu.
“Nilipokuwa nateua tume hii nilikuwa najua ugumu wa kazi, nilikuwa najua kuwa mtapata shida kwenda kuwahoji watu licha ya kwamba niliwapa uhuru wa kumhoji mtu yeyote na mmefanya kazi nzuri sana, kilichobaki sasa ni kuifanyia kazi,” alisema.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

JPM AKABIDHIWA RIPOTI YA UCHUNGUZI MALI ZA CCM
Reviewed by By News Reporter
on
5/22/2018 08:17:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: