Loading...
Naikumbuka kauli aliyowahi kuisema Rais Magufuli kuwa mwenye hila anaweza kukwambia neno lolote lile kutokana na chuki zake binafsi. Rais Magufuli alisema, “Hata ukiwa unaogelea, mwenye hila atakwambia unamtimulia vumbi”.
Nimeikumba kauli hiyo kutokana na kelele nyingi zilizopaswa wakati Serikali ilipotangaza kuongeza kodi kwenye sekta ya utalii wakasema tutapoteza Watalii na badala yake tushushe ili tuwe na ushindani vilivyo na nchi jirani, waliaminisha hivyo jamii kuwa utalii nchini utakwenda kupungua na hatimaye kufa kabisa.
Kadri siku zinavyozidi kwenda tunashuhudia idadi kubwa ya Watalii wakiongezeka kuja kutembelea nchini, tumeshuhudia mapato yatokanayo na utalii yakizidi kuongezeka pia. Akisoma hotuba ya makadilio ya Bajeti kwa Mwaka 2017/18 Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Khamis Kigwangalla amethibitisha hili la ongezeko la idadi ya Watalii nchini na mapato kuongezeka.
"Idadi ya watalii walioingia nchini imeongezeka kutoka watalii 1,284,279 kwa mwaka 2016 hadi kufikia watalii 1,327,143 kwa mwaka 2017, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.3. Watalii kutoka Marekani wameongoza katika kuitembelea Tanzania wakifuatiwa na nchi za Uingereza, India, Uholanzi na Uswisi," amesema Dkt. Kigwangalla.
Hali hiyo imesababisha Mapato yatokanayo na utalii yameongezeka pia kutoka Dola za Marekani milioni 2,131.57 kwa mwaka 2016 hadi kufikia Dola za Marekani 2,250.3 kwa mwaka 2017 ikiwa ni sawa na asilimia 5.6.
Kuongezeka kwa Watalii nchini kunatokana na mambo mbalimbali yakiwemo suala la amani na utulivu wa nchi yetu, uongozi bora, Sera safi za utalii pamoja utawala bora.
Nchi inazidi kusonga mbele, Watanzania tunazidi kuona matunda ya utawala wa Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

WATALII WAMEONGEZEKA, MAPATO YAMEONGEZEKA PIA
Reviewed by By News Reporter
on
5/21/2018 05:11:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: