Loading...
Waasi wa kundi la ADF wameendesha shambulizi Beni na kupeleka raia 10 kufariki. Waasi wa kundi la ADF kutoka nchini Uganda wameshambulia vijiji viwili Beni kabla ya kuondolewa na jeshi la serikali.
Taarifa kuhusu mashambulizi hayo imetolewa na shirika lisilokuwa na serikali Mashariki mwa Jamhuri ya kidemkrasia ya Kongo.
Kulingana na taarifa zilizotolewa ni kwamba waasi hao walivamia Jumapili vijiji vya Mangboko na Matapi katika ambali wa kilomita zaidi ya 20 na mji wa Beni.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Omar Kalisya , mkurugenzi wa shirika la kiraia la Mbau.
Waasi hao wameiba katika maduka tofauti katika vijiji hivyo kabla ya kukeleza mauaji na kuchomo moto magairi Jumapili.
Waasii hao ni wapinzani wa rais Museveni waliokimbia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kundi hilo la waaasi linathumiwa na Umoja wa Mataifa, serikali ya JK Kongo na asasi za kiraia kuendesha mauaji ya raia mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo tangu mwaka 2014.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WAASI KUTOKA BURUNDI WAUA RAIA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
Reviewed by By News Reporter
on
5/22/2018 09:30:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: