Loading...

KWA PICHA: MLIPUKO WA VOLKANO WAMEZA NYUMBA ZA WATU HAWAII, MAREKANI

Loading...
Milipuko ya volkano katika eneo la Kilauea, Hawaii imeharibu zaidi ya nyumba 26 na inatishia kuharibu nyumba nyingine mamia kadha.

Nyufa mpya zilitokea usiku maeneo hayo. Tayari watu zaidi ya 2,000 wamehamishwa makwao.

Baadhi waliruhusiwa kurejea Jumapili kuokoa wanyama wao, lakini maafisa wa serikali wanasema eneo hilo si salama.

Nyufa na mashimo mapya yalizuka usiku mtaa wa Leilani. Matope yenye moto yalirushwa futi 230 (mita 70) hewani.

Kisiwa hicho kilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 6.9 katika vipimo vya Richter Ijumaa.

Kilauea ni moja ya volkano zinazolipuka zaidi duniani. Imekuwa ikilipuka kwa miaka 35 sasa.
Baadhi ya maeneo, nyufa zinazofuka moshi zilizuka




Volkano ya Kilauea ililipuka Ijumaa, baada ya tetemeko la nguvu ya 6.9
Maafisa wanasema nyumba 26 zimeharibiwa kisiwani humo. Mamia zaidi zimo hatarini


Na Geofrey Okechi.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KWA PICHA: MLIPUKO WA VOLKANO WAMEZA NYUMBA ZA WATU HAWAII, MAREKANI KWA PICHA: MLIPUKO WA VOLKANO WAMEZA NYUMBA ZA WATU HAWAII, MAREKANI Reviewed by By News Reporter on 5/08/2018 09:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.