Loading...

USIWAZE SANA ANZA NA MATENDO

Loading...
Kuna wakati unahitaji kubadilika katika tabia fulani lakini inakuwa ni changamoto kwako kwa sababu tabia hiyo imeshaota mizizi ndani ya akili yako kiasi cha kupata shida kuishawishi akili katika kile ilichozoea.

Katika mazingira haya nini kifanyike? Je utawezaje kuibadili akili yako kupokea tabia mpya? Ni njia ipi sahihi ya kuvunja mizizi iliyokwisha jengeka ndani yako?. Akili ikishazoea tabia fulani si rahisi kukubali kupokea tabia nyingine mpya. Je mawazo chanya pekee yanatosha kuibadili akili yako kukuruhusu kujenga tabia mpya? Yawezekana! 


Lakini kitu rahisi kinachotakiwa kufanyika ili uweze kubadilika ni kuanza kuchukua hatua za matendo mapya ambayo ni sehemu ya hiyo tabia mpya unayoitaka bila kuangalia akili yako inasemaje. 
Usisubiri akili yako ikubaliane na wewe kuhusu hiyo tabia mpya bali anza kwa vitendo kwanza na akili yako itakufuata. Vitendo utakavyoanza kuvifanya vitaathiri fikra zako na kisha kuifanya akili ikubaliane na kile kinachoendelea.

Kadri unavyoendelea na matendo mapya ya tabia mpya mizizi ya tabia ya awali itaanza kukosa nguvu na mwisho tabia hiyo kupotea.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
USIWAZE SANA ANZA NA MATENDO USIWAZE SANA ANZA NA MATENDO Reviewed by By News Reporter on 5/07/2018 01:21:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.