Loading...

LULU DIVA NA RICH MAVOKO WAENDELEA KUFICHA PENZI LAO

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rich Mavoko na msanii mwenzake Lulu Diva wamedaiwa kuendelea kuficha penzi lao.

Kwa muda mrefu imekuwa ikisemekana kuwa Lulu DIva na Rich Mavoko ni wapenzi na hata tetesi hizo zimesapotiwa na picha zao mbali mbali ambazo zimekuwa zikionekana wakiwa pamoja.

Tetesi za wawili hawa kuwa pamoja zilianza tangu mwaka jana baada ya kudaiwa Lulu Diva ametoswa na mpenzi wake na hata mahari yake aliyotolewa kirudishwa baada ya kudaiwa kuchepuka na Mavoko.

Loading...
style="font-family: Verdana, sans-serif;">Baada ya kutoa wimbo wao unaoitwa 'Ona' unaofanya vizuri kwa hivi sasa wawili hao wamedai kuwa ukaribu wao ulikuwa kwa ajili ya kazi tu lakini hawana mahusiano yoyote zaidi ya urafiki wa kawaida.

Kwenye mahojiano na Mikito Nusunusu, Lulu Diva alisema kwamba, tetesi hizo si za kweli na zilitokana na watu kuunga baadhi ya video na picha na kuonesha kwamba wapo kwenye mahaba lakini si kweli, yupo karibu na jamaa huyo kwa sababu za kikazi.

"Mimi na Rich hatujawahi kuwa na uhusiano wowote, ni mtu wangu, tunasaidiana kwenye kazi, maana ndiye kanitungia hata wimbo wangu mpya wa Ona, kuhusu mapenzi hapana kiukweli".
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
LULU DIVA NA RICH MAVOKO WAENDELEA KUFICHA PENZI LAO LULU DIVA NA RICH MAVOKO WAENDELEA KUFICHA PENZI LAO Reviewed by By News Reporter on 5/21/2018 09:51:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.