Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema miundombinu ya kuunganisha bomba la gesi asilia, ikikamilika itapunguza kwa asilimia 40 gharama za gesi ya mitungi inayozalishwa nje ya nchi.
Dk Kalemani aliyasema hayo jana wakati akizindua ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha bomba la gesi asilia kutoka Mtwara inayotarajiwa kukamilika Septemba, uliofanyika eneo la Ubungo.
Alisema kwa sasa bei ya mtungi wa gesi kwa kuanzia ni kati ya Sh50,000 hadi 55,000 lakini kwa gesi asilia watapunguza asilimia 40 na itakuwa kati ya Sh20,000 hadi Sh30,000 kwa mtungi.
“Haya ni manufaa makubwa, nawahamasisha wananchi tena kwa msisitizo kutumia rasilimali ya gesi hii asilia kama nishati ya matumizi ya nyumbani badala ya kuni au umeme ambao ni gharama kubwa,” alisema Dk Kalemani.
Akitoa ushuhuda mkazi wa Mikocheni, Enerica Nyinje ambaye ni miongoni mwa wamiliki wa nyumba mbili zilizounganishwa na mfumo wa gesi hiyo kwa hatua za awali, alisema kuanza kutumia gesi hiyo kumempunguzia gharama.
Nyinje alisema awali alikuwa akitumia mtungi wa gesi wa kilo sita ambao aliujaza kwa Sh20,000 kwa mwezi, lakini baada ya kuunganishwa na mfumo wa g

Loading...
si asilia ndani ya wiki mbili ametumia Sh5,000.
“Nina uhakika ndani ya mwezi nitatumia Sh10,000 badala ya Sh20,000 kama ilivyokuwa awali,” alisema Nyinje.
Dk Kalemani alifafanua kuwa mita za ujazo trilioni 1.2 za gesi asilia zitatumika kusambazwa kwenye makazi ya watu, huku mita za ujazo trilioni 3.6 za gesi zitatumika kusambazwa viwandani na Sh11 bilioni zikitengwa kukamilisha kazi hiyo awamu ya kwanza ya mradi huo.
Alisema tayari wameanza rasmi kuunganisha bomba kubwa la gesi asilia kutoka bomba kubwa linalotoka Madimba Mtwara kuja Dar es Salaam, lenye urefu wa kilometa 7.8 kwa hatua ya kwanza, lakini litaendelea kutanuliwa kulingana na mahitaji ya wateja wa gesi hiyo.
Maeneo yatakayonufaika ni Mikocheni, Ubungo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza, Shekilango, Mwenge na Makongo Juu.
Naye kaimu mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kapuulya Musomba alisema kwamba Ubungo ndiko kutakapokuwa na matoleo ya kusambaza gesi hiyo kwenda sehemu mbalimbali.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

KIFURUSHI CHA GESI ASILIA KUWAFIKIA WATANZANIA MLANGONI
Reviewed by By News Reporter
on
5/21/2018 09:34:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: