Loading...

MITCHELLE OBAMA ASEMA HATAWANIA URAIS, AWASIHI WAMAREKANI WASIWATEGEMEE VIONGOZI KULETA MABADILIKO

Loading...
Mkewe rais mstaafu wa Marekani Barack Obama, Mitchelle Obama amewataka raia wa Marekani kupigania mabadiliko wanayohitaji na kuacha kuwategemea viongozi kuleta mabadiliko hayo. 

Akizungumza katika kongamano kuu la wanawake nchini Marekani siku ya Jumamosi, Mei 5 jijini Los Angeles, Mitchelle alisema kuwa raia wana uwezo wa kuleta mabadiliko hasa wanawake na kuwa viongozi hushirikiana nao kuyafikia malengo kwa bidii zao.

“Sitawania urais kwa sababu sijawahi kuwa na hamu ya kuwa mwanasiasa. Nina bahati ya kuolewa na mtu anayependa siasa na akanivutia huku. Ingawa nilitoa hotuba nzuri na mimi ni mwerevu, hivyo sio vigezo vya kumchagua rais. 

“Kuna wanawake wengi huko nje ambao wanapenda uongozi na siasa kwa mioyo yao. Huwezi kusema wewe ni mwanamke na sasa unaweza kuwania urais. Lazima mambo mengi yazingatiwe.” Mitchelle Obama alisema kwenye kongamano hilo kuu la wanawake lililohudhuriwa na takriba wajumbe 5,000.

Mitchelle alisema kuwa viongozi hawawezi kuleta mabadiliko ambayo watau wanahitaji, akisisitiza kuwa juhudi za watu binafsi ndizo huleta maendeleo. 

“Tusisubiri mtu mmoja atuokoe. Tulimpigia kura Barack Obama na hakumaliza ubaguzi wa rangi.” Mitchelle alinukuliwa na gazeti la Taifa Leo kuyasema hayo. 

Mkewe Obama alikuwa akijibu madai kuwa angewania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao na kusema kuwa hana mpango wa kuiongoza Marekani. Aidha Mitchelle alimsifu Hillary Clinton kwa kuwania kiti hicho licha ya kushindwa na rais wa sasa Donald Trump. Alimtaja Hillary kama mwaniaji aliyestahili kuwepo kwenye kinyang’anyiro hicho.

“Mwaniaji bora kwenye uchaguzi uliopita alikuwa mwanamke. Hakuna mkamilifu, lakini alikuwa na ukamilifu wa kipekee.

“Watu wengi hawakupiga kura. Sisi wanawake tunastahili kujiuliza, kwa nini? Ina maana kuwa bado hatujakubali uongozi tofauti, uongozi wa mwanamke.” Mitchelle alisema. 

Kongamano hilo kuu la 39 la wanawake nchini huwaleta pamoja wanawake kutoka majimbo tofauti nchini Marekeni kuzungumzia jinsi wanawake wanavyoweza kugeuza mitazamo yao ili kuwawezesha kuchangia katika maendeleo ya nchi.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MITCHELLE OBAMA ASEMA HATAWANIA URAIS, AWASIHI WAMAREKANI WASIWATEGEMEE VIONGOZI KULETA MABADILIKO MITCHELLE OBAMA ASEMA HATAWANIA URAIS, AWASIHI WAMAREKANI WASIWATEGEMEE VIONGOZI KULETA MABADILIKO Reviewed by By News Reporter on 5/08/2018 11:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.