Loading...

MVUA BADO IPO MPAKA MWISHONI MWA MWEZI

Loading...
MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA) imesema hali ya vipindi vya mvua itaendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa iliyotolewa na TMA jana ilieleza mwelekeo wa mvua kwa Mei 21-31 kwa Kanda ya Ziwa Victoria mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Mara itakuwa na vipindi vya mvua vitakavyoambatana na ngurumo za radi katika maeneo machache.

Aidha, mikoa ya Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro imetajwa kuwa na vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo machache.

Pia, Kanda ya Kati mikoa ya Dodoma na Singida na maeneo yake yataendelea kuwa makavu, taarifa ilisema, pamoja na mikoa ya Nyanda ya Juu Kusini-Magharibi mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa.

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa maeneo ya Kanda ya Pwani ya Kusini, mikoa ya Mtwara na Lindi, itakuwa na vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo machache, lakini mikoa ya Kanda ya Kusini mikoa ya Ruvuma na maeneo ya Kusini mwa Morogoro yatakuwa na hali ya mawingu.

Kadhalika,taarifa ilieleza katika kipindi hicho migandamizo mikubwa iliyopo kaskazini mwa dunia inatarajia kuendelea kudhoofika wakati ile ya kusini ikiendelea kuimarika.

“Ukanda wa mvua unatarajia kuendelea kusogea kuelekea kaskazini hali itakayopeleka upepo kuvuma kutoka kusini hadi kusini mashariki,” ilieleza taarifa hiyo.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa joto la bahari la wastani hadi juu kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo la kusini-magharibi mwa Bahari ya Hindi hali inayopunguza kutokea kwa vimbunga katika bahari.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MVUA BADO IPO MPAKA MWISHONI MWA MWEZI MVUA BADO IPO MPAKA MWISHONI MWA MWEZI Reviewed by By News Reporter on 5/23/2018 11:54:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.