Loading...
Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha (RUCU) kimesema pacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti watatafutiwa utaratibu mwingine wa kufanya mitihani yao, baada ya kutohudhuria masomo kwa takribani miezi mitano baada ya kuugua.
Pacha hao walisitisha masomo tangu Desemba 27 mwaka jana walipolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, kabla ya kuhamishiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Januari 4 mwaka huu na hivi karibuni kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango RUCU, Padri Kelvin Haule alisema jana kuwa kutokana na kukaa nje ya chuo kwa muda mrefu kwa matatizo ya kiafya, watatafutiwa utaratibu mpya.
Alisema wamesharudi Iringa na wapo chini ya uangalizi wa madaktari katika Hospitali ya Mkoa, lakini watakaporejeshwa chuoni uamuzi huo utakafanyika.
Pandri Haule alisema chuo kilifanya nao mazungumzo wakiwa hospitali miezi miwili iliyopita na waliweka bayana nia yao ya kuhamia fani ya kompyuta na kuachana na ualimu.
“Nilipoongea nao miezi miwili iliyopita walisema wanataka kuhama kutoka kwenye fani ya ualimu kwenda kompyuta kutokana na hali yao kiafya hawataweza kufundisha kwa urahisi,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema baada ya uchunguzi imebainika kuwa pacha hao hawahitaji upasuaji wowote kukamilisha matibabu yao.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

PACHA WALIOUNGANA KUTAFUTIWA UTARATIBU WA KUFANYA MITIHANI
Reviewed by By News Reporter
on
5/20/2018 11:29:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: