Loading...

PENZI LA ASLAY NA MAMA MTOTO WAKE LADAIWA KUVUNJIKA

Loading...
Kumekuwa na tetesi huko instagram kuwa msanii Aslay na mke wake ambae amebahatika kupata nae mtoto mmoja kuwa kwa sasa hawapo tena pamoja na kwamba wawili hao  kila mmoja anafata ustaarabu wake kwa saa na inawezekana hata kukaa pamoja hawakai tena.

Wikiendi hii ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa wawili hao huku siku zao zikiwa zimefatana  lakini kitu cha ajabu ni kwamba hakukuwa na shamrashamra za sherehe hiyo kwa wote wawili huku Aslay hakutaka hata kuweka picha ya mzazi mwenzake huyo katika ukurasa wake wa instagram

Habari ziliozpo chini ya kapeti ni kwamba Aslay na Tessy hawako pamoja tena na kwamba mwanamke huyo alishaondoka nyumbani kwa Aslay na sasa wapo katika mahuiano kama ya wazazi tu na sio vinginevyo.

Wasanii wengi wamekuwa na skendo za kuwa na mapenzi ya muda mfupi na pengine hata kushindwa kufikia muafaka wa ndoa kwa wapenzi wao huku swala kubwa likihusishwa na wivu wa mapenzi na kulewa umaarufu.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
PENZI LA ASLAY NA MAMA MTOTO WAKE LADAIWA KUVUNJIKA PENZI LA ASLAY NA MAMA MTOTO WAKE LADAIWA KUVUNJIKA Reviewed by By News Reporter on 5/08/2018 01:03:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.