Loading...

UWEUSI NI HALI YA AKILI

Loading...
Watu wengi weusi wanakabiliwa mtazamo duni kwa sababu wanalipa kipaumbele kwa kile ambacho wengine wanacho, hasa wazungu.

Wanajihisi hawajitoshelezi kwa kuangalia nyumba za wengine, samani, mavazi, magari na wadhifa.

Kitu ambacho mtu mwingine anafanya au anacho hakina maana yoyote kwako. Unapaswa kuacha wivu huo, mashindano na ushindani.

Unacho ulicho nacho. Kifurahie. Ni chako. Usitumie baraka zako kushindana na wengine kwa kujifananisha nao.

Wakati unashindana na kujifananisha na wengine, hatima yake ni kujisikia vibaya kwa wewe mwenyewe. Hauwezi kuwa na furaha.

Sio wazungu wote wanamali na utajiri mkubwa tunaoufikiria wengine ni maskini na hawajiwezi kuzidi hali tulizonazo.

Wengine wanafikia kukosa hadi sehemu za kuishi, huku wengine wakiwa wamepanga katika nyumba dhaifu na zakikabwela.

Namaanisha kwamba hatupaswi kujumuisha kwa mitazamo yetu kuwa wazungu wote ni mambo safi na kufikia kudharau rangi za ngozi zetu.

Na hili lisitufanye wanyonge au dhaifu katika mazingira au jamii tunazoishi.

Kuna mwanafalsafa mmoja na mwandishi wa Riwaya ya "No Exit" aliyoandika mwaka 1943, aliyefahamika kwa jina la Jean-Paul Sartre rais wa Ufaransa alishawahi kusema "Hell is Other people" akiwa na maana ya kuwa; Watu wanaokuzunguka ndio wanaokuwekea mipaka ya mitazamo yako.

Hii inathibitisha kuwa mtazamo juu ya rangi zetu za ngozi, wengine (Wazungu) ndio waliotubadili tuwe na mitazamo hasi na juu mwonekano wetu.

Kwahiyo bila wao na baadhi ya watu weusi kuendelea kudharau rangi ya ngozi zetu tusingekuwa wanyonge na kujiona hatuwezi katika namna ya kufanya maswala makubwa ya kimaendeleo.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
UWEUSI NI HALI YA AKILI UWEUSI NI HALI YA AKILI Reviewed by By News Reporter on 5/07/2018 11:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.