Loading...

WAZIRI MWAKYEMBE AMSIFIA FLAVIANA MATATA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amempongeza Mwanamitindo wa Kimataifa, Flaviana Matata kwa jitihada zake za kila siku katika kusaidia jamii.

Flaviana Matata ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Marekani ambapo ndipo anafanya kazi zake za uanamitindo amekuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi mbali mbali za kijamii.

Kwenye mazungumzo yake  na waandishi wa habari Jijini Dodoma Dkt. Mwakyembe amewataka vijana wa kitanzania kuiga mfano wa mwanamitindo huyo ili kuchangia katika uj
Loading...
nzi wa taifa.

"Nawasihi vijana wengine wenye fursa kama za Flaviana Matata kuzitumia vizuri kwa kuhakikisha jamii inanufaika na mafanikio waliyoyapata.

"Lakini pia Mwanamitindo huyo amekuwa ni Balozi mzuri katika kupeperusha bendera ya Taifa katika nchi mbalimbali za Ulaya".

Flaviana ameleza kuwa mbali na kujishughulisha na mitindo, ameweza kuanzisha kampuni ya Flaviana Matata Foundation ambayo inasaidia kutoa vifaa vya shule, ambapo hadi sasa amefanikiwa kutoa vifaa zaidi ya 5000 katika shule mbalimbali nchini.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WAZIRI MWAKYEMBE AMSIFIA FLAVIANA MATATA WAZIRI MWAKYEMBE AMSIFIA FLAVIANA MATATA Reviewed by By News Reporter on 5/18/2018 10:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.