Loading...

RUBANI MKUU KENYA AIRWAYS KUBURUZWA MAHAKAMI KISA MATUNZO YA WATOTO

Loading...
Mwanamke mmoja amshtaki rubani mkuu wa kampuni ya ndege ya Kenya Airways kwa kumtelekeza yeye na watoto wawili.

Doreen Nkatha Kirima, mwanamke mfanyabishara amemshtaki Bw. Japheth Mutisya Mutiso kwa kumuachia majukumu yote ya kifamilia peke yake.

Nkatha alidai rubani huyo alikaidi kuhudumia watoto ingawa ni mtu mwenye uwezo wa kutosheleza kuhudumia familia yake.

Kwa sababu hiyo, mwanamke huyo alidai kiasi cha Sh134,000 pesa za Kenya kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto wake wawili.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama wawili hao walikutana mwaka 2008 huko Donholm ambapo Nkatha alikuwa akiendesha duka la nafaka ambapo Mitisya alikuwa akienda dukani hapo kwa mteja wa mara kwa mara.

Alidai ijapokuwa hawakuwa kuishi kama mke na mume lakini mahusiano yao yalizaa matunda na kubahatika kupata watoto wawili, ikiwa mtoto wao wa kwanza alizaliwa mwaka 2012. Tokea hapo rubani huyo alihudumia watoto hao mpaka ilipofika mwaka 2017 wakati amesafiri kwenda Hong Kong na familia yake ya kwanza na aliacha kuwasiliana na mimi.

"Alipoendelea kuzuia mawasiliano yangu, nikachukua maamuzi ya kuwasiliana na mkewe na mke wake alinishauri niende kufungua kesi ya madai ya matunzo ya watoto, ili niweze kupata haki zangu kisheria," nyaraka za mahakama zilieleza.
Na Peter Godwin



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RUBANI MKUU KENYA AIRWAYS KUBURUZWA MAHAKAMI KISA MATUNZO YA WATOTO RUBANI MKUU KENYA AIRWAYS KUBURUZWA MAHAKAMI KISA MATUNZO YA WATOTO Reviewed by By News Reporter on 6/08/2018 06:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.