Loading...

ASKOFU MKUU KANISA KATOLIKI AUSTRALIA AFUNGWA JELA MIAKA 12

Loading...
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Australia, amefungwa jela miezi 12 kwa kutoripoti kesi za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto miaka ya 1970, zilizofanywa na kasisi wa Kanisa hilo.

Philip Wilson, amepatikana na kosa hilo na anakuwa mmoja wa viongozi wa Kanisa hilo duniani ambaye amepatikana na kosa hilo.

Mahakama hata hivyo, imesema kuwa Askofu huyo atazuiwa nyumbani kwa muda huo wote.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Australia alijiuzulu baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya kuficha kashfa za ulawiti iliyokuwa ikimuandama.

Philip Wilson, Askofu Mkuu wa Adelaide, kusini mwa Australia anakuwa afisa wa kwanza wa ngazi za juu wa Kanisa Katoliki kushtakiwa na kuhukumiwa kutokana na kashfa za ngono zinazolizunguka kanisa hilo kwa miongo mingi sasa.
Na Salma Omari.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ASKOFU MKUU KANISA KATOLIKI AUSTRALIA AFUNGWA JELA MIAKA 12 ASKOFU MKUU KANISA KATOLIKI AUSTRALIA AFUNGWA JELA MIAKA 12 Reviewed by By News Reporter on 7/03/2018 11:06:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.