Loading...

UMOJA WA AFRIKA WAKUBALIANA KUSHUGHULIKIA SUALA LA WAHAMIAJI

Loading...
Viongozi wa Umoja wa Afrika wamekubaliana kuunda bodi maalum itakayosaidia, kushughulikia masuala ya wahamiaji lakini pia kuthathmini sera za uhamiaji katika mataifa ya Afrika.

Tume hiyo pia inatarajiwa kutafuta mbinu za kuimairisha uhusiano kati ya mataifa ya kigeni kuhusu masuala ya uhamiaji.

Hii imekuja wakati huu waafrika wengi wakiendelea kukimbilia barani Ulaya, huku wengi wakizama katika Bahari ya Mediterania wakiwa njiani.

Hayo yanajiri wakati ambapo wahamiaji 63 wamezama katika Bahari ya Meditterenian Pwani ya Libya, wakiwa njiani kwenda barani Ulaya.

Hata hivyo, wahamiaji wengine 41 waliokolewa, katika meli hiyo iliyokuwa na abiria zaidi ya 100.

Kati ya siku ya Ijumaa na Jumamosi wiki, iliyopita, mamia ya wahamiaji walizama na maafisa wanasema zaidi ya 100 hawajapatikana.

Raia wengi kutoka Afrika ambao wamekua wakielekea ulaya kutafuta maisha mazuri walikumbwa na mikasa mingi, huku baadhi yao wakipoteza maisha kutokana na jali mbalimbali zilizokua zikiwakumba katika maeneo wanakopita hasa baharini.
Na Hamisi Fakhi.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
UMOJA WA AFRIKA WAKUBALIANA KUSHUGHULIKIA SUALA LA WAHAMIAJI UMOJA WA AFRIKA WAKUBALIANA KUSHUGHULIKIA SUALA LA WAHAMIAJI Reviewed by By News Reporter on 7/03/2018 11:01:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.