Loading...

BETWAY YAFADHILI SHS 20 MILIONI TAMASHA LA GOLDEN HEART LA BEBE COOL

Loading...
Kampani ya bahati nasibu, Betway ya nchini Uganda imetangaza kushirikiana na msanii wa miondoko ya regge, Bebe Cool kwa kumchangia kiasi cha Milioni 20 pesa za Kiganda kuhakikisha anafanikisha tamasha lake kwa ajili ya kuchangia watoto wenye matatizo ya moyo.

Tamasha hilo linatarajiwa kuanza rasmi tarehe 3, Agosti katika ukumbi wa Serena Conference Hall.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Adellah Agaba, meneja wa Betway nchini Uganda alisema; "Kama kampuni, tumeguswa na posti ya Bebe Cool ya 26 Juni, 2018. Staa huyo wa regge baada ya kutusimulia hali ya mtoto Sheila, ambaye anahitajika kuperekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi ili apone baada ya upasuaji wa mara ya kwanza kukosa matumaini."

Kuhakikisha tamasha hilo hilo linafanyika, kampuni hiyo ya bahati nasibu imejitolea kiasi cha Shilingi milioni 20 pesa za kiganda ili kukamilisha tukio.

"Kiasi hiki kitalipia matibabu ya mtoto Sheila na watoto wengine watano kwa ajili upasuaji wa kunusuru maisha yao," Agaba aliongezea.

Bebe Cool aliweka wazi kuwa; hii ni mwanzo tu wa tamasha la Golden Heart. Kwa mujibu wa nyota huyo, atawasafirisha watoto 5 kila tamasha litakapo fanyika kuhakikisha ananusuru maisha ya watoto hao.

Walengwa watasafirishwa wiki mbili baada ya tamasha kufanyika, Tamasha tiketi zake zitauzwa kwa shilingi laki 1 pesa za kiganda na 5 milioni kwa tiketi za mezani, na tiketi zitaanza kuuzwa kuanzia julai 10.
Na Marry Timoth.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BETWAY YAFADHILI SHS 20 MILIONI TAMASHA LA GOLDEN HEART LA BEBE COOL BETWAY YAFADHILI SHS 20 MILIONI TAMASHA LA GOLDEN HEART LA BEBE COOL Reviewed by By News Reporter on 7/03/2018 10:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.