Loading...

MBUNGE AZICHAPA NA AFISA WAKE MSAIDIZI KISA MSHIKO

Loading...
Kwa kawaida urafiki na pesa huwa haviambatani kabisa na hata kitabu kitakatifu kinapeana mwongozo dhabiti ambapo pia kinaonya kuwa pesa ni chanzo cha maovu yote.

Kuna picha ambayo imeenezwa mitandaoni ikiwaonyesha viongozi wawili wakilimana makonde mbele ya bosi wao bila kujali.

Inasemekana mbunge mmoja ambaye anajulikana sana kwa kupigana vita dhidi ya ufisadi tangu serikali za awali na afisa mmoja msaidizi wa mwanasiasi maarufu walikuwa wakizozana kuhusu marupuru kabla ya kuanza kuzabana makofi na kulimana magumi hadi sakafuni.

Kulingana na habari tulizozipokea hapa kutoka mtandao mmoja huko Kenya, mbunge huyo alimkashifu afisa msaidizi kwa kutomlipa marupurupu yake baada ya kufanya kampeni ya kisiasa nje ya Nairobi.

"Mbunge alikuwa akidai malipo yake baada ya kuandamana na mwanasiasa mashuhuri kufanya kampeni za kisiasa nje ya Nairobi, kwa kila mara huwa wanalipwa marupurupu kwa kuzuru maeneo kadhaa ya nchi wakizindua miradi na kuomba kura. Mbunge huyo alikuwa ameghadhabishwa sana na afisa msaidizi wa mwanasiasa huyo na kupelekea kumzaba makofi na kulimana magumu mbeli ya bosi wao,' Shahidi alisema.

Habari za kuaminika ziliarifu kuwa mbunge huyo anawakilisha eneo bunge moja jijini Nairobi na anajulikana kuwa mtetezi mkuu wa uongozi bora na huwa mstari wa mbele kupigana vita dhidi ya ufisadi.

Mbunge huyo anasemekana kuwa miongoni mwa wacheshi wa zamani ambaye alikuwa akitumia ucheshi wake kukemea ufisadi tangu wakati wa utawala wa rais mstaafu Daniel Moi.

"Karibu wawili hao wauane mbele ya bosi wao, kilikuwa kisa cha aibu sana ambacho kilitulizwa na viongozi wenye maadili ambao walikuwa wamemtembelea mwanasiasa huyo afisini mwake," Shahidi aliongezea.

Afisa huyo msaidizi anasemekana kuwa jeuri na katili kupindukia na pia anajulikana kwa kumtetea bosi wake sana kiwango cha kuitwa nywila yake.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MBUNGE AZICHAPA NA AFISA WAKE MSAIDIZI KISA MSHIKO MBUNGE AZICHAPA NA AFISA WAKE MSAIDIZI KISA MSHIKO Reviewed by By News Reporter on 7/08/2018 12:33:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.