Loading...

TABIA 5 ZA KUIGA KWA WATU WALIOFANIKIWA MAISHANI

Loading...
Kila mtu analenga kufanikiwa maishani. Malengo ya mafanikio ni mambo ambayo yanaambatana na bidii, uvumilizu na ukakamavu wa hali ya juu wa mtu.

Tumewasikia watu wengi waliofanikiwa wakieleza jinsi walivyolazimika kujinyima sana ili kufika walipo leo.

Wengine huamka mapema sana na kulala kwa kuchelewa wakijaribu kutimiza ndoto zao maishani. 

Ukimwona mtu anamiliki jumba kubwa, magari ya kifahari, kampuni zenye umaarufu na kupata mishahara mikubwa, sio wazi kuwa alishiriki ufisadi kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu hapa nchini. 

Wengi wao watakuarifu walivyojituma kuyapata waliyo nayo kwa kuwa na nguzo za kuwaelekeza.

Ikiwa una talanta, wapenda biashara au wewe ni msomi na ukose mwongozo wako na mwelekeo, basi utajiri wako wa kibinafsi unaweza kukosa kukupa mafanikio maishani. 

DundiikaNews imefanya utafiti na kukuandalia orodha ya tabia tano walizo nazo watu waliofanikiwa:

1. Ari ya kufanikiwa 

Watu waliofanikiwa huwa na mshawasha wa kuafikia malengo yao kwa vyovyote vile. 

Wana hamu ya kile wanachokitaka na wao hujaribu sana kukipata. 

2. Kutumia muda vizuri 

Waliofanikiwa wana mazoea ya kutumia kila dakika katika maisha yao vizuri. 

Hawawezi kupoteza dira kwa sababu ya kitu chochote na wanatumia muda wao vizuri kwa kupanga kazi zao kwa njia nzuri. 

3. Hawapotezi dira kwa malengo yao 

Watu waliofanikiwa hutenga muda, rasilimali na mawazo yao kufanikisha malengo yao, bila ya kupoteza mwelekeo kwa sababu ya kitu chochote, kiwe kikubwa au kidogo. 

Wanawaza sana kwa upana ili kubuni mbinu watakazotumia kuafikia malengo hayo 

Wao huhakikisha kuwa wametimiza malengo yao, tofauti na watu wa kawaida ambao huwa na malengo na kukosa kuyatimiza na hilo haliwatatizi mawazo.

4. Ni watu wa kujituma 

Watu walionawiri kwenye mafanikio hawasubiri kupata mafanikio kwa bahati au kusaidiwa, bali wao hutafuta mafanikio kwa njia zozote zilizo mbele yao. 

Wao ni watu ambao wanatambua umuhimu wa kutangulia kulifanya jambo ili kupata mafanikio makubwa. 

Kwa hali zetu za kibinadamu, kujituma ni kumwomba Mola afanikishe mipango yako huku ukijikakamua kuyafanikisha kwa njia zozote utakazopata. 

5. Wanajifunza mambo mapya kila siku 

Ni wazi kuwa yeyote anayekoma kujifunza mambo mapya amakata pumzi akiwa hai, hivyo watu waliofanikiwa hujifunza mambo mapya kila wakati kwa kuwa wanaamini hawajui kila kitu. 

Hali hiyo huwasaida kukua kibinafsi, hivyo wanaweza kugeuza mawazo yao na hali ya maisha kulingana na mambo ambayo wanaangazia kufanikisha maishani. 

Hii inajumuisha kurejelea masomo au kozi fupifupi ili kuwa na elimu ya maswala tofauti.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TABIA 5 ZA KUIGA KWA WATU WALIOFANIKIWA MAISHANI TABIA 5 ZA KUIGA KWA WATU WALIOFANIKIWA MAISHANI Reviewed by By News Reporter on 7/08/2018 11:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.