Loading...

VERA SIDIKA NA BROWN NDOA INANUKIA

Loading...
Baadhi wamedai kuwa Sosholaiti Vera Sidika anautumia uhusiano huo kujipa umaarufu na huku wengi wa kidai kuwa anajaribu kulisafisha jina lake baada ya fununu kuzagaa kuwa anauza mwili wake kwa vigogo.

Vera alipoulizwa kuwa kama yupo tayari kufunga pingu za maisha na msanii huyo, alijibu kwa ujanja.

"Kwa sasa siwezi kuahidi hilo kwa kuwa mambo yanaweza kutokea na sijui nini kitatokea mbele yetu," Vera alinukuliwa.

Alieleza kuwa uhusiano wake wa awali ulisambaratika licha ya kujua kuwa wangeonana rasmi na jamaa huyo.

"Kwa mfano, uhusiano wangu uliopita ulikuwa ukielekea kwenye mkondo huo wa ndoa lakini baadaye ikatokea kwamba kulikuwa na mapungufu fulani hivyo mipango hiyo tukafutilia mbali," aliongezea.

Amethibitisha kuwa uhusiano wao u shwari na iwapo ndoa itatokea hana budi na pia ikisambaratika, si neno.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VERA SIDIKA NA BROWN NDOA INANUKIA VERA SIDIKA NA BROWN NDOA INANUKIA Reviewed by By News Reporter on 7/08/2018 11:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.