Loading...

WAKAZI WATAKA HATUA ZICHUKULIWE BAADA YA SIMBA KUUA NG'OMBE HUKO NYERI - KENYA

Loading...
Wakazi wa kijiji cha Gatuanyaga katika jimbo la Kieni, kata ya Nyeri wameitaka Mamlaka ya huduma ya wanyama pori ya Kenya (KWS) kuwasaka Simba watano waliosababisha vifo vya ng'ombe watano.

Simba hao, wanashukiwa kuzagaa maeneo ya karibu na Solio Ranchi, walivamia kijiji kimoja na kuanzia kufanya mauaji hayo hadi saa 10 alfajiri kufika na wanakijiji walipoanza kuwatimua.

Tukio hilo limewashtua wanakijiji baada ya kuanza kufananisha matukio ya upotevu wa mifugo zaidi ya 100 kwa kipindi cha miezi mitatu na tukio hilo la simba kuvamia kijijini kwao.

Mwanakijiji mmoja kwa jina la Francis Githinji, ambaye amepoteza ng'ombe wawili wenye thamani ya pesa za Kenya Sh170,000 amewalaumu KWS askari wa wanyama pori kushindwa kuwalinda wanyama hatari kama simba wasiingie katika mazingira ya watu.

Ila mpaka sasa askari wa wanyama pori wameweza kukamata simba mmoja na jitihada za kuwashika wote zinaendelea.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WAKAZI WATAKA HATUA ZICHUKULIWE BAADA YA SIMBA KUUA NG'OMBE HUKO NYERI - KENYA WAKAZI WATAKA HATUA ZICHUKULIWE BAADA YA SIMBA KUUA NG'OMBE HUKO NYERI - KENYA Reviewed by By News Reporter on 7/08/2018 10:49:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.