Loading...

RAIS MAGUFULI KUWAONGOZA WATANZANIA KWENYE MAPOKEZI YA NDEGE BOEING 787-8 DREAMLINER

Loading...
RAIS Dkt. John Magufuli leo Jumapili Julai 08, 2018 atawaongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa alasiri ya leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Rais, Gerson Msigwa na kusema ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 mchana ikiwa inatokeaa Seattle nchini Marekani.

Hii ni ndege ya nne kuwasili nchini kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuimarisha huduma zake.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS MAGUFULI KUWAONGOZA WATANZANIA KWENYE MAPOKEZI YA NDEGE BOEING 787-8 DREAMLINER RAIS MAGUFULI KUWAONGOZA WATANZANIA KWENYE MAPOKEZI YA NDEGE BOEING 787-8 DREAMLINER Reviewed by By News Reporter on 7/08/2018 10:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.