Loading...

ATCL YAKANUSHA UVUMI JUU YA UBOVU WA NDEGE YA DREAMLINER

Loading...
Kampuni ya ndege ya ATCL wametolea ufananuzi kuhusu uhairishwaji wa safari zake katika ndege yake mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner, ambayo inaruka na kufanya masafa yake mikoa ya Dar es salaam, Mwanza na Kilimanjaro.

Akitoa ufananuzi kwa njia ya simu alipokuwa akizungumza katika mahojiano na gazeti la Citizen, Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ATCL afisa Ladislaus Matindi amekanusha uvumi kwamba ndege hiyo imehairisha safari zake kwa sababu za kiufundi, ambao ulionea kwenye mitandao ya kijamii.

Ameweka wazi kwamba ndege hiyo imesimamisha shughuli zake kwa muda, lakini kwa lengo la kukamilisha mahitaji ya kiufundi.

Kwa mujibu Bw Matindi, Dreamliner inafanyiwa matengenezo ya muda hususani katika mfumo wa Wi-Fi.

Alielezea zaidi na kusema hata marubani wanapewa mafunzo zaidi ili wawe na uzoefu wa safari za nje lakini uvumi wa ndege mbovi ni za uzushi na sio kweli, na baada ya hayo kukamilika ndege hiyo itaendelea na safari zake kama kawaida.
Na Geofrey Okechi.





Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ATCL YAKANUSHA UVUMI JUU YA UBOVU WA NDEGE YA DREAMLINER ATCL YAKANUSHA UVUMI JUU YA UBOVU WA NDEGE YA DREAMLINER Reviewed by By News Reporter on 8/18/2018 12:20:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.