Loading...

KIJANA AIDUKUA APPLE KWA SABABU ALITAKA KUFANYA NAO KAZI

Loading...
Kijana mmoja kutoka nchini Australia amekiri kuudukua mtandao wa Apple na kuiba nyaraka kadhaa.

Kijana huyo wa kiume mwenye miaka 16 aliingia kwenye mtandao huo mara kadhaa mwaka huu kutoka nyumbani kwao huko Melbourne, Australia kwa mujibu wa gazeti la Age,

Alisema alihifadhi nyaraka hizo kwenye ghala linalofahamika kama 'hacky hack hack'.

Apple inasema kuwa hakuna taarifa za wateja wake zilivuja.

Lakini gazeti la Age linasisitiza kuwa kijana huyo aliingia kwenye akaunti za wateja.

Mdukuzi maarufu
Kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa mahakamani, kampuni ya simu ililijulisha shirika la ujasasi la Marekani wakati ilifahamu kuhusu udukuzi huo na kuwajulisha polisi wa Australia AFP.

Polisi hao kisha wakafanya uvamizi kwenye nyumba ya kijana huyo ambapo walipata kompiuta mbili zenye namba sawa na za vifaa vilivyotumiwa. Polisi pia walipota simu na vifaa vingine.

Kwa mujibu wa Age, kijana huyo alikuwa amejigamba kuhusu udukuzi huo kwenye ujumbe wa WhatsApp. Age liliripoti kuwa alidukua kwa sababu alikuwa shabiki mkubwa wa Apple na alikuwa na ndoto ya kufanya kazi huko.

Wakili wake alisema alikuwa amepata umaarufu mkubwa kwenye jhamii ya wadukuzi duniani.

Jina la kijana huyo halijafichuliwa kwa sababu za kisheria. Atahukumiwa tarehe 20 Septemba.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KIJANA AIDUKUA APPLE KWA SABABU ALITAKA KUFANYA NAO KAZI KIJANA AIDUKUA APPLE KWA SABABU ALITAKA KUFANYA NAO KAZI Reviewed by By News Reporter on 8/18/2018 11:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.