Loading...

EPL UPDATES: CHELSEA MWENDO MDUNDO, YAICHAPA NEWCASTLE UTD 2 - 1

Loading...
Chelsea leo imepambana kuhakikisha inapata ushindi ugenini St James Park  mbele ya kocha wao wa zamani, Rafael Benitez baada ya kufanikiwa kuichapa Newcastle United mabao 2-1. 

Chelsea ndio ilikua ya kwanza kupata goli kupitia kwa staa wake Eden Hazard dakika ya 76 kwa mkwaju wa penati kabla ya Joselu kuisawazishia Newcastle dakika ya 83. Shuti la jioni lake beki Marcos Alonso lilimbabatiza deAndre Yedlin na kujifunga na hivyo kuwapa uhakika wa pointi tatu vijana hao wa darajani. 

Kwa matokeo hayo Chelsea inayonolewa na muitaliano Maurizio sarri wamechupa hadi nafasi ya pili wakiwa na alama tisa sawa na Liverpool inayoongoza kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
EPL UPDATES: CHELSEA MWENDO MDUNDO, YAICHAPA NEWCASTLE UTD 2 - 1 EPL UPDATES: CHELSEA MWENDO MDUNDO, YAICHAPA NEWCASTLE UTD 2 - 1 Reviewed by By News Reporter on 8/27/2018 06:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.