Loading...
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Soni wamejiuzulu nafasi hizo, leo Jumanne Agosti 28, 2018.
Ghasia ambaye ni mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) na Soni (Babati Vijijini), wametangaza uamuzi wao huo leo asubuhi mjini Dodoma mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.
Mtandao mmoja wa habari hapa nchini ulizungumza na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai kuhusu kujiuzulu kwa viongozi hao na kubainisha kuwa ni kweli wamejiuzulu.
"Ni kweli wamejiuzulu nafasi zao na mimi sijajua kwa nini wamejiuzulu,” amesema.
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mtandao wa DundiikaNews kujua nini sababu hasa ya kujiuzulu.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HABARI ZA HIVI PUNDE: GHASIA AJIUZULU UENYEKITI KAMATI YA BUNGE YA BAJETI
Reviewed by By News Reporter
on
8/28/2018 02:26:00 PM
Rating:
![HABARI ZA HIVI PUNDE: GHASIA AJIUZULU UENYEKITI KAMATI YA BUNGE YA BAJETI](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgthzt8urT88Shu5rYTmXY8ZjpPLUFLba9O2etAdyNvf2fiO5aR0ScqYHvk0pljldTHQeGbkcw7-Vhc3ENPTkafGzCkaa-7oWAG2O9lGvSA409zDN_pmJaDrk6i3cc2TE7hdDi5najh4kc/s72-c/hawa+ghasia+ajiuzulu+nafasi+yake.jpg)
Hakuna maoni: