Loading...

MCHEZAJI WA ZAMANI WA TIMU YA UINGEREZA ALAZWA HOSPITALINI BAADA YA KUNG'ATWA NA PANYA

Loading...
Mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza, Gary Mabbutt amesema panya amekula sehemu ya mguu (katika unyayo) wakati alipokuwa amelala katika mapumziko yake huko Afrika Kusini.

Mchezaji, 57, alilazimishwa kurudi nchini kwake Uingereza kwa ajili ya operesheni na alilazimika kukaa wiki nzima hospitalini hapo. Mabbutt ambaye pia anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari alikabiliwa na maumivu makali katika unyayo wake.

Tukio hilo lilitokea wiki 6 zilizopita wakati alipomtembelea binti yake, ambaye anafanya kazi katika hifadhi ya wanyama ya Kruger.

"Nilikwenda kulala na ilipofika usiku panya alikuja katika chumba changu cha kulala, akapanda kitandani na aliamua kung'ata unyayo wangu," alisema Mabbutt.

"Alinichimba kishimo kikubwa katika kisigino changu, mpaka karibu na mfupa wa mguu wangu. Alimng'ata pia mtoto wangu kidole gumba katika chumba chake kabla ya panya huyo kuja kwangu."

Alidai panya anang'ata kwa ustadi wa hali kiasi ambacho alishindwa kugundua kama anang'atwa na panya.

Mabbutt amesema anahitaji matibabu ya kila siku kuakikisha anatibu jeraha lake.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MCHEZAJI WA ZAMANI WA TIMU YA UINGEREZA ALAZWA HOSPITALINI BAADA YA KUNG'ATWA NA PANYA MCHEZAJI WA ZAMANI WA TIMU YA UINGEREZA ALAZWA HOSPITALINI BAADA YA KUNG'ATWA NA PANYA Reviewed by By News Reporter on 8/28/2018 02:47:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.