Loading...

JESHI LA (JWTZ) KUADHIMISHA MIAKA 54 TANGU KUANZISHWA KWA KUFANYA USAFI

Jeshi la Wananchi Tanzania ( JWTZ) limesema linajivunia kuendelea kulinda amani ya watanzania kwa nidhamu ya hali ya juu kwa muda wa miaka 54 sasa tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo mwaka 1964.

Kauli hiyo,imetolewa mapema jana jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa habari na uhusiano wa Jeshi hilo Kanali Ramadhani Dogoli, wakati alipokua akitoa taarifa ya maadhimisho ya kutimiza miaka 54 kwa jeshi hilo.

Amesema kuwa,kutokana na uwezo huo jeshi hilo limekuwa likitumiwa na Umoja wa Mataifa( UN) katika kutuliza ghasia kwa nchi zenye machafuko ya amani ikiwemo nchi ya DRC Kongo,na nchi ya Sudan.
Loading...
justify;">
Aidha ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya usafi katika maeneo yao siku ya septemba mosi mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya maadhimisho ya miaka 54 tangu kuanzishwa kwake.

“Nawaomba wananchi wajijitokeze kwa winging ufanyaji usafi katika maeneo yao, kwa upande wa jeshi lao limeanza tangu Agosti 27 mwaka huu, kushiriki shughuli mbalimbali za usafi kwenye maeneo ya kambi zote za jeshi pamoja na kufanya michezo mbalimbali Vikosini”amesema Dogoli.

Ikumbukwe kuwa Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ huazimisha kumbukumbu ya kuanzishwa kwake mwaka1964 baada ya kubadilishwa jina kutoka Tanganyika Rifle (TR) ambalo lilikua jeshi la wakoloni.
Na Habiba Rashid.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JESHI LA (JWTZ) KUADHIMISHA MIAKA 54 TANGU KUANZISHWA KWA KUFANYA USAFI JESHI LA (JWTZ) KUADHIMISHA MIAKA 54 TANGU KUANZISHWA KWA KUFANYA USAFI Reviewed by By News Reporter on 8/30/2018 11:10:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.