Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako, ametoa wito kwa wataalam wa somo la hesabu kuja na mbinu mpya ya kufundishia ili kumaliza ufaulu mbovu wa wanafunzi katika somo hilo.
Alisema ni vibaya kuona kwamba miaka 10 iliyopita wastani wa ufaulu mpaka sasa umeshindwa kuvuka asilimia 20.
Akiongea na wataalam wa somo la hesabu kutoka nchi mbalimbali duniani katika kikao kilichofanyika katika Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo jijini Dar es Salaam, Prof Ndalichako amesema ni aibu kuona asilimia 80 ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kila mwaka wanashindwa kufaulu somo la hesabu.

Loading...
na" , sans-serif;">
"Kama serikali, hatutoruhusu asilimia 80 ya wanafunzi kufeli somo la hesabu kila mwaka. Kwanini wanafeli hivi?" aliuliza waziri, aliongezea kwamba kufeli kwa somo la hesabu matokeo yake ni kuzalisha walimu wachache.
"Nawataka nyinyi na mimi tuvunje mzunguko huu. Kama walimu na wakufunzi wanakimbia hesabu, hao watakaobakia hawawezi kukidhi haja. Na mwisho wa siku tutaendelea kuwa na uhaba wa walimu kila mwaka," alisema Prof Ndalichako.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

WATAALAMU WA SOMO LA HISABATI WATAKIWA KUJA NA MBINU MPYA ZA KUFUNDISHIA
Reviewed by By News Reporter
on
8/30/2018 12:01:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: