Mtu yeyote makini anajua kwamba kuwa na dhumuni (ndoto) kwenye maisha unayoiamini ni sawa na kuwa na mtoto.
Utamjali. Utamlinda. Utatumia muda mwingi kumfikiria, kuwa na wasiwasi naye, kumlea akue. Ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Swali linakuja Je! ni kwanini hatakiwi kukata tamaa? hizi ni sababu za msingi kabisa;
- Unapokata tamaa, unaendelea kujibebesha mzigo wa kushindwa katika maisha yako ya baadae. Utaendelea kufikiria hali ile ile kila wakati. Utaghadhabika. Na utahisi majuto na pale utakapokutana na changamoto zile zile utakuwa mtu wa kuhairisha tu, mwishowe hautofanikisha lolote lile.
- Kukata tamaa kutakufanya upunguze kasi ya uzalishaji katika shuguli zako za kila siku, kwakuwa ukiwaza ile hali ya kukata tamaa itakula nguvu zako za ziada na hata kupunguza kasi ambayo ungeitumia katika uzalishaji mali.
- Kukata tamaa kunakaribisha kushindwa katika maisha, hivyo basi swala likiwa gumu ukikata tamaa utajiona umeshindwa.
- Kukata tamaa, kunakaribisha na kuchochea tabia kwa waliokuzunguka kama jamaa, ndugu na marafiki. Hivyo basi ukiruhusu leo kukata t
Loading...
maa kesho huenda mwanao naye akarithi tabia yako kwa kukuona baba au mama ulishindwa jana.
- Kukata tamaa kunashusha heshima yako, kama utashiriki mradi fulani na wenzako halafu ukaonyesha hali ya kukata tamaa, kwa muda mwingine hawatokuamini hata kama fursa ilikuangukia wewe.
- Unapoteza imani juu yako, kwa sababu utajiuliza maswali mbele ya safari itakapotokea unataka kufanya swala gumu na mwishowe utashindwa tena.
- Inadhoofisha afya ya akili yako, kwasababu kukata tamaa kunaperekea kujiona haujitambui.
Kwa vyovyote vile, haupaswi kukata tamaa - kwa sababu utaua ndoto zako kubwa na kupoteza dira na muelekeo wa maisha yako.
~ "Kabla haujakata tamaa, fikiria kwanini ulishikilia jambo hilo kwa muda sana."
Na Mariam Kalisa.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KWANINI HAUPASWI KUKATA TAMAA?
Reviewed by By News Reporter
on
8/30/2018 12:19:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: