Loading...

AFRIKA KUSINI: JULIUS MALEMA ATAKA KISWAHILI IWE LUGHA RASMI BARANI AFRIKA

Kiongozi wa chama cha watetezi wa Uhuru wa kiuchumi (EFF) cha Afrika Kusini, Julius Malema, ametoa wito wa kupitishwa kwa lugha moja itakayotumika barani Afrika, huku akipendekeza lugha ya Kiswahili kuwa lugha hiyo.

Malema aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na EFF, ambapo aliongelea mambo mbalimbali ikiwemo ujumbe wa Rais wa Marekani kwenye mtandao wa Twitter kuhusu marekebisho ya sheria ya ardhi Afrika Kusini.

"Tunatakiwa k
Loading...
zalisha lugha moja ambayo itatumika kwenye bara zima. Kwa mfano Kiswahili, kinaweza kukuzwa ili kitumike barani kote" alisema Malema.

Lugha ya kiswahili ni lugha inayotumika sana barani Afrika, ambapo kinatumika sana Afrika mashariki na kati. Ni lugha rasmi kwa nchi ya Tanzania na Kenya.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
AFRIKA KUSINI: JULIUS MALEMA ATAKA KISWAHILI IWE LUGHA RASMI BARANI AFRIKA AFRIKA KUSINI: JULIUS MALEMA ATAKA KISWAHILI IWE LUGHA RASMI BARANI AFRIKA Reviewed by By News Reporter on 8/30/2018 12:37:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.