Loading...

MCHEZAJI MKONGWE WA TIMU YA BRAZIL MBIONI KUWA RAIS WA REAL VALLADOLID KWA UWEKEZAJI WA BILIONI 80

Mchezaji maarufu wa Brazil Ronaldo analenga kuwa rais wa klabu ya kandanda ya Uhispania, Real Valladolid baada ya kuwekeza kwenye hisa za thamani ya euro €30 milioni sawa na 80 bilioni pesa za Kitanzania, ambapo amekuwa mshikadau mkuu katika klabu hiyo.

Kulingana na ripoti ya UK Daily Mail kulingana na programu ya radio ya Uhispania El Larguero, mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid ndiye atakuwa rais wa klabu hiyo baada ya uwekezaji huo mkubwa.

Ripoti hiyo ilieleza kuwa rais wa sasa Carlos Suarez, atasalia kuwa meneja mkurugenzi wa klabu hiyo. 

Loading...
dana, sans-serif;">Katika suala la kufurahisha, mkataba huo umemaliza miezi ya majadiliano kati ya Valladolid na Ronaldo ambapo mchezaji wa zamani wa Inter Milan na raia wa Mexico na mfanyibiashara mashuhuri Ernesto Tinajero atakuwa mmiliki wa klabu hiyo.

Valladolid imerejea tena katika ligi ya Uhispania na imepata matokeo changamani, baada ya kutoka droo na Girona na kushindwa kwa kiwango kidogo na Barcelona. 

Awali, Ronaldo alitangaza azimio la kuendesha klabu Uhispania au Uingereza kabla ya kujiunga na shirikisho la kandanda la Brazil. Lakini alisema angependa kwanza kuendesha klabu kubwa.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MCHEZAJI MKONGWE WA TIMU YA BRAZIL MBIONI KUWA RAIS WA REAL VALLADOLID KWA UWEKEZAJI WA BILIONI 80 MCHEZAJI MKONGWE WA TIMU YA BRAZIL MBIONI KUWA RAIS WA REAL VALLADOLID KWA UWEKEZAJI WA BILIONI 80 Reviewed by By News Reporter on 8/30/2018 10:17:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.