Loading...

KANYE WEST AMZAWADIA KIM KARDASHIAN GARI LA KIFAHARI, NEON MERCEDES

Loading...
Kim Kardashian West amejikuta akitumbukia katika matairi manne ya kipekee baada ya kupewa zawadi ambayo hakuitarajia.

Kanye West, 41, amempatia mkewe, 37, gari la kifahari ya mtindo wa Mercedes G series SUV aina ya neon yenye rangi ya kijani, ambayo wawili hao waliikodi huko nyuma walipokuwa mjini Miami - Marekani.

"Nilikuwa nikitoka kufanya mazoezi nikajikuta nikipewa zawadi ya kushtukizwa. Naipenda sana gari hii nilipokuwa Miami, na nilikuwa nikiizungumzia muda wote," alisema Kardashian West, ambaye alifunguka hisia zake kupitia ukurasa wake wa Instagram mwisho wa wiki.

Gari hiyo aliyopewa zawadi na Kanye inafanana na ya mdogo wake Kylie Jenner lakini yake ni rangi ya chungwa.
Na Haika Gabriel.






Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KANYE WEST AMZAWADIA KIM KARDASHIAN GARI LA KIFAHARI, NEON MERCEDES KANYE WEST AMZAWADIA KIM KARDASHIAN GARI LA KIFAHARI, NEON MERCEDES Reviewed by By News Reporter on 8/27/2018 07:47:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.