Loading...
Mwanamuziki mwanasiasa Bobi Wine ambaye amekuwa akizuiliwa kwa karibu wiki mbili nchini Uganda ameachiliwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu, kaskazini mwa nchi hiyo.
Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi amepewa dhamana pamoja na wabunge wengine watatu, na watuhumiwa wengine wanane.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuhusika katika kurushia mawe magari ya msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Arua.
Kassiano Wadri aliyeshinda ubunge Arua ni miongoni mwa wabunge waliokuwazuiliwa.
Bw Wadri ameachiliwa kwa dhamana lakini akazuiwa kuzuru eneo bunge lake kwa miezi mitatu bila idhini ya mahakama.
Maombi ya dhamana ya washukiwa wengine 21 walioshtakiwa pamoja na Bobi Wine yatasikilizwa na mahakama baadaye leo.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MBUNGE NA MWANAMUZIKI BOBI WINE AACHILIWA HURU KWA DHAMANA
Reviewed by By News Reporter
on
8/27/2018 01:39:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: