Loading...

NYOTA WA TENNIS SERENA WILLIAM APIGWA MARUFUKU KUVAA MAVAZI YANAYOMBANA WAKATI WA MECHI

Loading...
Nyota wa Tennis, Serena Williams, amepigwa marufuku kuvaa vazi lililomkaba(bodysuit) wakati wa mashindano ya French Opens.

Nyota huyo alivaa nguo hiyo aliporejea Grand Slam Roland Garros Mei, miezi kadhaa baada ya kujifungua bintiye Septemba 2017.

Williams alishinda Kristyna Pliskova katika mzunguko wa kwanza wa French Open, na kueleza kuwa alihisi vizuri kuvaa vazi hilo kwani lilimfanya kuhisi kama ‘shujaa’.

"Ninaishi katika ulimwengu wangu, nilitaka kuwa shujaa, na ni njia yangu ya kuwa shujaa,” alisema kuhusiana na vazi hilo. 

Lakini rais wa French Tennis Federation Bernard Giudicelli alisema shirikisho hilo halitakubali nguo kama hiyo na kuwataka wachezji kuheshimu mchezo huo.

Kuna mpango wa kuzindua sheria na kanuni mpya na njia ya kuvaa wakati wa mchuano. 

“Kwa mfano, nguo ya Serena mwaka huu haitakubaliwa,” alisema. Inasemekana binti huyo alikumbwa na matatizo wakati wa kuzaa bintiye, Alexis Olympia Ohanian Jr, na ndio maana alikuwa akivaa nguo kama hiyo.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
NYOTA WA TENNIS SERENA WILLIAM APIGWA MARUFUKU KUVAA MAVAZI YANAYOMBANA WAKATI WA MECHI NYOTA WA TENNIS SERENA WILLIAM APIGWA MARUFUKU KUVAA MAVAZI YANAYOMBANA WAKATI WA MECHI Reviewed by By News Reporter on 8/28/2018 10:10:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.