Loading...

MAJINA WAGOMBEA URAIS DRC KUTANGAZWA 19 SEPTEMBA

Loading...
Raia wa DRC wanasubiri majina ya wagombea watakaowania urais mwezi Desemba. Lakini bado mgawanyiko umeendelea kujitokeza upande wa upinzani ambao wanajaribu kutafuta mgomba mmoja pekee ambaye atapambana na mgombea wa chama tawala na washirika wake katika uchaguzi huo.

Tayari Tume ya Uchaguzi (CENI) imesema watu 25 waliomba kuwania urais, kumrithi rais Joseph Kabila ambaye hatawania tena.

Majina ya wagombea wa mwisho yatatangazwa tarehe 19 mwezi Septemba.

Mgombea wa chama tawala cha PPRD anatatrajiwa kuwa Waziri wa zamani wa Mambo Emmanuel Ramazani Shadary, huku ikisubiriwa kuona iwapo wapinzani wanaungana na kuwa na mgombea mmoja.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAJINA WAGOMBEA URAIS DRC KUTANGAZWA 19 SEPTEMBA MAJINA WAGOMBEA URAIS DRC KUTANGAZWA 19 SEPTEMBA Reviewed by By News Reporter on 8/13/2018 11:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.