Loading...

WANAJESHI WA NIGERIA WAFYATA MKIA KWA WANAMGAMBO YA BOKO HARAM

Loading...
Baadhi ya wanajeshi wa Nigeria wamegoma kwenda vitani kukabiliana na Boko Haram, baada ya kufyatua risasi angani kupinga amri ya kwenda mstari wa mbele kukabiliana na kundi hilo.

Vyombo vya habari nchini Nigeria vimethibitisha hali hiyo na kuripoti kwamba mgomo huo uliendelea kwa takribani saa nane.

Kwa mujibu wa mashahidi askari walikataa kupanda ndege ambayo ilikuwa iwahamishe kutoka Maiduguri kwenda katika mji wa Marte karibu na nchi jirani ya Niger katika vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.

Hatu hiyo ya wanajeshi hao iliwashangaza wengi baada ya kukaidi amri ya uongozi wa jeshi wa kwenda vitani kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram.

Kwa mujibu wa chanzo cha jeshi nchini humo ambacho hakikutaja jina lake, hali ya kutotii amri miongoni mwa wanajeshi imeendelea kwa miaka nane sasa.

Jeshi la Nigeria limekua likikabiliana na kundi la Boko Haramu kwa miaka kadhaa, huku raia wakiendelea kuwa na hofu kufuatia hali yao ya usalama.
Na Neema Bushubo.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WANAJESHI WA NIGERIA WAFYATA MKIA KWA WANAMGAMBO YA BOKO HARAM WANAJESHI WA NIGERIA WAFYATA MKIA KWA WANAMGAMBO YA BOKO HARAM Reviewed by By News Reporter on 8/13/2018 11:32:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.