Loading...

MBOSSO AMTAKA RICH MAVOKO AJE NA USHAIDI WA UNYONYAJI WA WASAFI

Loading...
Msanii kutoka WCB mbosso amefunguka kwa waandishiwa habari na kusema kuwa msanii rich  mavoko ambae amekuwa akitangaza kuwa WCB wanafanya kazi ya unyonyaji kwa wasanii wao ni uongo na kama kweli basi aje na kitu cha kuthibitisha maneno yake kama ni kweli.

Mbosso anasema kuwa kwa muda wote aliokuwa akifanya kazi wasafi mpaka sasa anaona kabisa kuwa hajarudisha hata robo ya kile alitakiwa kukirudisha kwa mambo ambayo amefanyiwa na WCB kwa muda wote.

"mimi tangu nianze kuingiza kazi wasafi, sinaona kama nimerudisha mema niliyofanyiwa na WCB,  ile ela waliyowekeza kwangu bado sijarudisha hivyo nikiambiwa kuwa nina nyonywa kwakweli binafsi nitakataa kwa sababu naona mimi ndio ninawanyonya wao.

"kwaio unaponiambia kuwa Mbosso unanyonywa WCB basi uje na ushaidi kuwa nina nyonywaje."

Wasafi ina wasanii wengi sana ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya lebo hiyo lakini, Rich ni msanii wa kwanza kutoka WCB huku akisema kuwa sababu kubwa ni unyonyaji unaofanywa na wasafi katika kufanya kazi na malipo kwa wasanii wao.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MBOSSO AMTAKA RICH MAVOKO AJE NA USHAIDI WA UNYONYAJI WA WASAFI MBOSSO AMTAKA RICH MAVOKO AJE NA USHAIDI WA UNYONYAJI WA WASAFI Reviewed by By News Reporter on 8/14/2018 09:57:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.