Loading...

TETEMEKO LA ARDHI INDONESIA: WATU ZAIDI 430 WAPOTEZA MAISHA

Loading...
Tetemeko la ardhi lililopiga kisiwa cha Lombok nchini Indonesia Agosti 5 imesababisha watu zaidi ya 430 kupoteza maisha. Shughuli ya kutafuta watu walioffunikwa na udongo au kukwama chini ya vifusi linaendelea.

Tetemeko hilo la ardhi pia limesababisha uharibifu wa vitu na mali vyenye thamani ya dola milioni 350i, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa Jumatatu wiki hii na taasisi inayokabiliana na Majanga nchini humo (BNPB).

Zaidi ya watu 350,000 walilazimika kuyahama makaazi yao kwa wakati mmoja.

"Uharibifu na hasara ni kubwa," amesema Sutopo Nugroho, msemaji wa taasisi inayokabiliana na Majanga (BNPB).

Jumatatu wki hii rais wa Indonesia Joko Widodo amezuru maeneo yaliyokumbwa na tukio hilo.

Ameomba kuimarisha shughuli za upelelezi na uokoaji, kwa kuzingatia maeneo ambako wanaweza kupatikana watu waliotoweka.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TETEMEKO LA ARDHI INDONESIA: WATU ZAIDI 430 WAPOTEZA MAISHA TETEMEKO LA ARDHI INDONESIA: WATU ZAIDI 430 WAPOTEZA MAISHA Reviewed by By News Reporter on 8/14/2018 10:09:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.