Loading...

TAFITI: MAZOEZI YA KILA SIKU HUSAIDI AFYA YA AKILI

Loading...
Mazoezi ya kila siku yanasaidia kwa kiasi kikubwa afya ya akili.

Viwango vya shughuli za kimwili na hali ya kisaikolojia ya watu milioni 1.2 vimefanyiwa utafiti nchini Marekani.

Utafiti huo umegundua kwamba mazoezi kama michezo ya timu, mafunzo ya baiskeli na mazoezi ya aerobic, ambayo yalitolewa mara 3 hadi 5 kwa wiki kwa muda wa dakika 45, yalileta mabadiliko katika akili.

Utafiti huo umegundua kwamba shughuli zote za kimwili, ikiwemo kazi za nyumbani na shughuli za kuhudumia watoto, zilikuwa nzuri kwa afya ya akili bila kujali umri wala jinsia.

Ilielezwa kuwa dakika 30 hadi 60 za shughuli za kimwili mara moja katika kila siku mbili zina manufaa zaidi.
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TAFITI: MAZOEZI YA KILA SIKU HUSAIDI AFYA YA AKILI TAFITI: MAZOEZI YA KILA SIKU HUSAIDI AFYA YA AKILI Reviewed by By News Reporter on 8/14/2018 10:16:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.