Loading...

MIAKA MITANO JELA KWA KUMFANYIA MTIHANI MWANAFUNZI WAKE

Loading...
Benjamin Manirambona, mwalimu mkuu ambaye alikamtwa akimfanyia mtihani wa taifa mwanafunzi wake amehukumiwa miaka 5 jela huko Burundi.

Bw. Manirambona, Mwalimu Mkuu wa shule ya Buterere, alikamatwa siku ya Ijumaa tarehe 10 Agosti wakati akijaribu kumfanyia mtihani mmoja wa wanafunzi wake.

Baadae alipelekwa rumande chini ya ulinzi wa polisi mpaka ilipofika juzi Jumanne tarehe 14 Agosti huku wakisubiri muafaka wa hukumu ya kesi yake. Aliburuzwa mahakamani pamoja na wenzake wawili mmoja ni muhasibu wa shule ya Buterere Bw. Eric Nkurunziza na mwingine ni katibu wa muhasibu Lazarre Nihezagire.

Muendesha mashtaka alipendekeza kwamba Benjamin Manirambona anapaswa kuhukumiwa miaka 12 jela na kulipa faini ya BIF 200,000 pesa za Burundi, baada ya kesi kuamuliwa alihukumiwa miaka 5 jela na miaka 10 bila kufanya shughuli yoyote ya umma.

Lazarre Nihezagire na Eric Nkurunziza wali wamehukumiwa miaka 2 na nusu jela na miaka 5 bila kufanya shughuli zozote za umma.

Wakati alipokamatwa, Bw. Manirambona alisema alikuwa anamfanyia mtihani wa kielectronikia kwa niaba yake mwanajeshi anayedumisha amani huko Somalia.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MIAKA MITANO JELA KWA KUMFANYIA MTIHANI MWANAFUNZI WAKE MIAKA MITANO JELA KWA KUMFANYIA MTIHANI MWANAFUNZI WAKE Reviewed by By News Reporter on 8/17/2018 08:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.