Loading...

MISRI YAZIDI KUKAZA UZI SHERIA YA UHALIFU WA MTANDAO

Loading...
Rais wa nchi ya Misri Abdel Fattah al-Sisi ametia saini sheria mpya inayobana matumizi ya mtandao.

Sheria ya "Uhalifu wa mtandao" humaanisha kwamba tovuti yeyote inaweza kuzuiliwa ndani ya mipaka ya Misri kama itakuwa na lengo la kuathiri usalama na uchumi wa nchi hiyo kiujumla.

Mamlaka zimesema mapitio mapya yanahitajika kufanyika ili kumaliza uvunjifu wa usalama na ugaidi.

Lakini makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu wameishutumu serikali kwa kujaribu kumaliza upinzani wa kisiasa.

CAFTE wamesema kufikia hadi sasa zaidi ya tovuti 500 zimekwisha zuiliwa baada ya sheria hiyo kutiwa saini.
Na Mary Mkeu.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MISRI YAZIDI KUKAZA UZI SHERIA YA UHALIFU WA MTANDAO MISRI YAZIDI KUKAZA UZI SHERIA YA UHALIFU WA MTANDAO Reviewed by By News Reporter on 8/19/2018 12:25:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.