Loading...

WATU WAZIMA WASIOVUTA SIGARA, WANAHATARI KUBWA YA KUPATA KANSA YA MAPAFU KAMA WAZAZI WAO WALIKUWA WAVUTAJI - TAFITI

Loading...
Watu wazima wasiovuta sigara wapo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha yao kwa ugonjwa hatari wa kansa ya mapafu kama tu walilelewa na wazazi waliokuwa wanavuta sigara, kulingana na utafiti uliofanywa Marekani.

Watafiti walisema watoto waliokuwa wakivuta moshi wa sigara kwa njia ya uvutaji wa wazazi au walezi wao "Ni sawa na kuongeza vifo vya watu 7 kwa kila watu wazima 100,000 wasiovuta sigara wanaokufa kwa mwaka".

Wataalam wanasema njia bora ya kuwalinda watoto ni kuacha kuvuta sigara.

Kama watu wazima wataishi na wavutaji wa sigara katika makazi yao, kuna tatizo jingine la kiafya litaibuka, utafiti umeonyesha.

Kama utavuta moshi wa sigara kwa muda wa masaa 10 na zaidi kila wiki inaongeza hatari ya kufariki kwa magonjwa ya moyo kwa 27%, Kiharusi kwa 23%, Magonjwa tata ya mapafu kwa 42% kulinganisha na wasioishi na wavutaji wa sigara.

Utafiti huu ndio wakwanza kuhusisha wazazi/walezi wanaovuta sigara na madhara atakayopata mtoto kiafya baada ya kuwa mtu mzima.
Na Neeema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WATU WAZIMA WASIOVUTA SIGARA, WANAHATARI KUBWA YA KUPATA KANSA YA MAPAFU KAMA WAZAZI WAO WALIKUWA WAVUTAJI - TAFITI WATU WAZIMA WASIOVUTA SIGARA, WANAHATARI KUBWA YA KUPATA KANSA YA MAPAFU KAMA WAZAZI WAO WALIKUWA WAVUTAJI - TAFITI Reviewed by By News Reporter on 8/19/2018 11:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.