Loading...

VISA NA MIKASA: WAZEE WAWILI WASHIKWA NA KUTAIHIRIWA KWA LAZIMA

Loading...
Wanaume wawili wametahiriwa kwa lazima katika soko la Soy katika mpaka wa kaunti za Uasin Gishi na Kakamega nchini Kenya.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, jamaa wa kwanza mwenye umri wa miak 47 aliyetambulika kama Michael Iremi alitahiriwa bila hiari yake Alhamisi, Agosti 9 mbele ya wanaume wengine waliokuwa wametahiriwa.

‘’Kundi la vijana walimkamata Iremi ambaye ni wa jamii ya Turkana alipotoka kazini akielekea nyumbani ,’’ John Inyangala, mkazi wa Soy Market aliiambia mtandao wa TUKO. Aidha, alieleza kuwa kundi hilo lilimkamata mzee wa jamii ya Luo mwenye umri wa miaka 50 aliyetambulika kama Oduor Jumamosi, Agosti 11 na kumtahiri kwa lazima vile vile.

Alieleza kuwa Oduor alitahiriwa huku amelala chini baada ya kukataa kusimama kulingana na tamaduni ya Bukusu. 

Video fupi iliyosambazwa katika mtandao wa twitter ulimuonyesha Oduor akiwa amelala chini akiwa uchi na mwili wake ukipakwa matope huku amezingirwa wana kundi la vijana wanaoziimba nyimbo za Bukusu za Kutahiri.

Inyangala aliliambia jarida moja maarufu la nchini Kenya - TUKO kuwa Oduor anaendelea kupata nafuu nyumbani kwa mwajiri wake. 

''Baadhi ya wenyeji walimchangia pesa. Hali yake imeimarika. Amekuwa akiwaepuka wanaotaka kumtahiri kwa muda mrefu,’’ Ingangala alisema.

Kamishna wa kaunti ya Trans Nzoia Erastus Mbui aliwaagiza machifu kuhakikisha kuwa hakuna yeyote anayelazimishwa na mila hiyo.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: WAZEE WAWILI WASHIKWA NA KUTAIHIRIWA KWA LAZIMA VISA NA MIKASA: WAZEE WAWILI WASHIKWA NA KUTAIHIRIWA KWA LAZIMA Reviewed by By News Reporter on 8/19/2018 10:31:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.