Loading...
Kampuni ya sukari Kilombero Sugar iliyopo mkaoni Morogoro, imewahakikishia watanzania kuwa ina shehena kubwa ya bidhaa hiyo inayoweza kutumika mwaka mzima, hivyo wananchi wasitarajie kutokea kwa uhaba wa bidhaa hiyo kama ilivyotokea miezi michache iliyopita.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo GUY WILLIAM amebainisha hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya kampuni hiyo ya kitanzania ambapo itamwezesha mwananchi wa hali ya chini kumudu gharama za ununuaji kwa bei nafuu.
Amesema bidhaa hiyo mpya ni baada ya kugundua mahitaji makubwa ya wananchi waliowengi ambao wamekua waathirika wakubwa wa bei pindi sukari inapoadimika sokoni.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
SAKATA LA SUKARI NCHINI LAPATIWA UFUMBUZI
Reviewed by By News Reporter
on
8/26/2018 02:10:00 PM
Rating:
![SAKATA LA SUKARI NCHINI LAPATIWA UFUMBUZI](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdIVVCtzM6iHo16JpXIbMY_9_8w3i7sNKhwnKuctCtSCk97z4wY13fcmpDjde74sCLDpI-GG2BmNdk_DBUy9yB1mrfydk47QLonyx_-1Udh29BjiLXxo_PW_QMZSCm29gwcvY5BwWsDo8/s72-c/sukari+tatizo+lakwisha.jpg)
Hakuna maoni: